Mkurugeni mtendaji wa GGM (wa pili kulia) Bw. Terry Mulpeter akimuonyesha Naibu Waziri Mhe. Luhaga Mpina (katikati), bwawa linalotumika kusambaza maji safi katika mji wa Geita
faini hiyo inatokana na kosa la kukosa vyoo vya wafanyakazi zaidi ya mia tatu (300) katika eneo la chini ya ardhi underground la uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Hali hiyo imeipelekea NEMC kuutoza mgodi huo faini ya shilingi milioni 10, zinazotakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne.
Katika ziara hiyo iliyomlazimu Naibu Waziri Mpina kuvaa vifaa maluum ili kuweza kuingia katika eneo la chini ya ardhi lenye mwamba mkubwa wa mgodi huo, akiambatana na baadhi ya maafisa aliongozana nao katika ziara yake, Naibu Waziri alijionea namna ambavyo eneo lenye idadi kubwa ya wafanyakazi kukosa huduma hiyo muhimu ya choo inayowapelekea kujisaidia vichakani na kuharibu mazingira.
Sehemu ya chini ya ardhi (underground) yenye dhahabu ya mgodi wa GGM inayosemekaka kukosa huduma ya choo kwa watumishi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya mia tatu, ikionekana kwa nje
Aidha Naibu Waziri Mpina pia aliweza kujionea uharibifu mwingine unaofanywa na mgodi huo wa utiririshwaji wa Maji ya mvua yaliyochanganyikana na madawa hatarishi kwa mazingira na viumbe hai kwenda kwenye makazi ya wananchi.
Kufuatia hali hiyo, Naibu waziri Mpina alielekeza uongozi wa mgodi huo kujenga miundombinu rafiki kwa mazingira yatakayopelekea maji hayo kwenda katika mkondo sahihi.
Bw. Simon Mushy Makamu wa Rais wa Mgodi wa GGM akijibu maswali ya Naibu Waziri
Akiongea kwa Niaba ya GGM makamu wa Rais wa Mgodi huo Bw. Simon Mushy, alisema kuwa wapo kwenye mchakato wa kujenga miundombinu kwa kushiriana na Halmashauri ya Mji wa Geita.
Kwa upande wa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Katoma Bi. Magori James Katoka alisema kuwa vumbi na maji ya mvua vinavyotoka kwenye mgodi huo vimekuwa ni kero na changamoto ya muda mrefu katikma kijiji hicho.
Pamoja na malalamiko mengi ya wakazi wa Katoma Geita kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa na mgodi wa GGM, Mgodi huo pia umefanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusambza maji safi a salama katika mji wa Geita ukishirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka ya Mkoa huo.
Sehemu ya kutupia na kutetekeza taka ngumu katika mgodi wa GGM Geita.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina Katika Mkoa wa geita ni muendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira, viwanda na migodi nchini.
Bwawa la majitaka la Mgodi wa dhabu wa Geita wa Geita Gold Mining maarufu kama GGM, ambapo imeelekezwa kuweka mabomba ya kusafisha majitaka hayo kuingia katika mabwawa.