Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo
Mkurugenzi wa Taifa wa Sensa na Takwimu za Jamii katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw, Ephraim Kwesigabo amesema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Kwesigabo amesema ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa gharama za bidhaa za vinywaji baridi na vyakula ikiwemo mchele, unga, nyama, samaki huku mwenendo wa mafuta ukibadilika.
Hata hivyo Bw, Kwesigambo amesema pia mabadiliko hayo hayajaathiri gharama za maisha na kuongeza kuwa mfumuko wa bei haujapanda nchini Tanzania pekee ila na nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda.
Kwa mujibu wa Kwesigabo amesema kupanda kwa mfumuko wa bei unaathiri uwezo wa shilingi ya Tanzania kununua bidhaa na kuwa mfumuko ukipanda uwezo wa shilingi huporomoka.
Aidha amefafanua kuwa mfumuko wa bei katika kipindi kama hiki mwaka jana ulikuwa ni asilimia 5.9 ukilinganisha na asilimia 6.3 ya sasa.