Jumamosi , 7th Jul , 2018

Meya wa mji wa Broummana nchini Lebanon Pierre Achkar amewaajiri warembo wa vyuo vikuu katika kitengo cha maafisa usalama barabarani huku akiwapa mashariti ya kuzingatia.

Mabinti wa vyuo waliojiriwa na Jeshi la Polisi nchini Lebanon.

Pierre ametoa nafasi hiyo kwa mabinti wa vyuo vikuu kuajiriwa ili kufanya kazi na maafisa usalama barabarani huku akiwataka kuvaa nguo fupi kwa kile alichodai kuwa ni sehemu ya kuvutia vyombo vya habari, ndani na nje ya nchi.

"Sababu kubwa ya kuajiri mabinti hawa ni kuongeza mvuto katika maeneo yetu ya mji na kuvutia vyombo vya habari ambapo tutapata namba kubwa ya watalii na kukuza uchumi wa nchi yetu”, amesema Pierre.

Hili ni agizo la pili kutoka kwa Pierre baada ya siku chache zilizopita kutoa agizo kwa walimu wa mazoezi ya viungo kufundisha mabinti pembezoni mwa barabara mjini Broummana ili kuwavutia watalii.