Jumatano , 26th Feb , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa Meya wa Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob, anatamani kuhamia CCM ambapo amemuambia kuwa, CCM hawapigani ngumi na kwamba yeye atawasumbua tu.

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Meya wa Ubungo CHADEMA, Boniface Jacob.

Makonda ameyabainisha hayo wakati akifungua mkutano wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC), ambapo baada ya kutomuona Meya huyo ndani ya kikao alimuagiza Meya wa Kinondoni ampigie simu ili awahi kusikiliza mambo ya msingi na siyo baadaye achelewe akaende kulalamikia twitter.

"Jacob naye alikuwa anatamani tamani kuja huku kwetu, mimi nikamuambia sisi utatusumbua maana CCM hatupigami ngumi, amezoea kila pahala kusimama kama baunsa na ule mwili sasa unaongezeka tu, anachelewa kwenye vikao mambo ya msingi yanapita, baadaye utamuona yuko twitter uko anahangaika tu" amesema Makonda.