Jumatatu , 30th Mei , 2016

Mbunge wa Mikumi Mkoani Morogoro Joseph Haule CHADEMA ameiomba serikali kujenga barabara ya Kilosa hadi Mikumi ambayo ni kilomita 78 kwa kiwango cha lami kwani ni kichocheo kikubwa sana cha maendeleo.

Haule maarufu kama Prof. J ameyasema hayo Bungeni Dodoma wakati wa maswali na majibu na kuitaka serikali itoe kauli ya kujenga barabara hiyo ambayo pia itaunganisha kata za eneo hilo.

Aikiju swali hilo Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Edwin Ngonyani amesema kwamba serikali inatambua suala hilo na barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami.

''Natambua juhudi zako Mbunge Haule na umeshakuja hadi ofisini kuulizia barabara hii nataka nikuhakikishie kama mlivyopitisha bajeti , barabara hii itajengwa''Amesema Naibu Waziri Ngonyani.