Jumatano , 4th Jun , 2014

Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha mapinduzi CCM nchini Tanzania Mh. Magreth Mkanga ameikumbusha serikali kuhakikisha kwamba inatenda haki kwa watu wenye ulemavu hasa katika masuala ya upatikanaji wa huduma za afya.

Huduma za msingi kama baiskeli za magurudumu matatu ni muhimu na haki kwa watu wenye ulemavu wa viungo.

Mh. Mkanga amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati alipokuwa akichangia hotuba ya makadiria ya bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii.

Amesema serikali imewasahau watu wenye ulemavu katika kuwapatia haki zao za msingi licha ya kuishauri serikali mara kwa mara kuhusu watu wenye ulemavu na hivyo amezishauri idara husika husika kulichukua suala hilo na kulipeleka ofisi ya waziri mkuu ambayo ndio itamudu kutatua matatizo yanayowakabili watu wenye ulemavu.