
Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Marwa Chacha Ryoba
Akizungumza na www.eatv.tv Ryoba amesema licha ya kuwa katika chama kimoja, bado hajabadilisha msimamo wake dhidi ya Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa bado anatamani achukuliwe hatua na mamlaka zilizomteua.
‘Mahusiano yangu na Mkurugenzi ni mazuri kwa sababu tuko chama kimoja, na wala sijawahi kumsingizia hata kimoja, nilichokisema kiko hivyo hivyo mpaka kesho kutwa, na naamini vyombo vya uchunguzi vitatoa majibu,” amesema Ryoba.
“Kimsingi yule Mkurugenzi ni rafiki yangu, na tuko vizuri lakini tunapofikia kwenye jambo la kiutendaji huwa lazima tuwajibishane japo safari hii siwezi kumchongea tena nitafuata taratibu za uwajibishaji,” ameongeza.
Septemba mwaka huu alipokuwa Mbunge wa CHADEMA, Marwa Ryoba alitoa madai juu ya mkurugenzi huyo mbele ya mkutano wa Rais Magufuli kwa kueleza kuwa amekuwa na matumizi mabaya ya fedha kwenye halmashauri hiyo.