Mbowe afiwa na Kaka yake 

Alhamisi , 8th Jul , 2021

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe, amefiwa na Kaka yake ajulikanaye kwa jina la Charles Mbowe.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe

Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo Julai 8, 2021, na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, kupitia ukurasa wake wa Twitter, wakati alipotumia mtandao huo kutoa salamu za pole kwa familia.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Charles Mbowe , Kaka ya Mwenyekiti Freeman Mbowe, poleni sana familia ya Kaka Charles na ukoo wote wa Mbowe, Mwenyezi  Mungu awe mfariji wenu wakati huu wa majonzi na ampumzishe marehemu mahali pema," ame-tweet Mh. Mnyika.