Jumanne , 17th Dec , 2019

Kesho Disemba 18, 2019 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wanatarajiwa kuchagua Mwenyekiti wao wa Taifa pamoja na Makamu Mwenyekiti, ambapo Wajumbe zaidi ya 1000 watashiriki Mkutano huo.

Mwenyekiti wa CHADEMA anayemaliza muda wake Freeman Mbowe.

Katika Uchaguzi huo nafasi ya Uenyekiti inawaniwa na wabunge wawili ambao ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe.

Katika nafasi ya makamu Mwenyekiti, inawaniwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, huku Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea,akitangaza kujiondoa jana kwa kile alichokisema Tundu Lissu ndiye anafaa zaidi.

Jana Disemba 16, 2019, kwenye Mkutano na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mawasiliano Itifaki na Mambo ya Nje (CHADEMA), John Mrema alisema majina ya wagombea wote yanapelekwa leo katika kikao Cha Baraza Kuu kwa