
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, wakati akizungumza na BBC Swahili
Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na BBC Swahili, ambapo ameongeza kuwa kwa kipindi chote hicho upelelezi wa kesi zake ulikuwa bado haujakamilika lakini wapo wenzake katika kesi hiyo uchunguzi ulikwishakamilika na wanatumikia hukumu zao.
"Mbowe kipindi kirefu hakuwepo nchini, alikuwa Nairobi, lakini alivyoingia tu nchini akaitisha maandamano na madai ya Katiba, nadhani ni calculations akijua kwamba ana kesi ya aina hiyo na hii vurugu anayoifanya akikamatwa aseme mmh! kwa sababu ya Katiba, lakini kwa vile jambo lipo mahakamani sina uhuru wa kulizungumzia nadhani tuiachie Mahakama zioneshe ulimwengu kwamba hizo shutuma ni za kweli ama si za kweli," amesema Rais Samia.