Jumamosi , 29th Jul , 2023

Marekani imesema kuwa inamuunga mkono rais aliyeondolewa madarakani nchini Niger Mohamed Bazoum baada ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewaonya wale wanaomzuia Bw Bazoum kwamba mamia ya misada mamilioni ya dola za kimarekani ipo hatarini.

Mkuu wa kitengo cha ulinzi wa rais Jenerali Abdourahmane Tchiani amejitangaza kuwa kiongozi mpya wa Niger. Bwana Bazoum alikuwa akichukuliwa kama mshirika muhimu wa mataifa ya magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu katika eneo hilo.

Kunaonekana kuna wasiwasi katika nchi za Magharibi kuhusu ni nchi gani kiongozi mpya atakubaliana nazo. Majirani wa Niger, Burkina Faso na Mali, wote wameikosoa Urusi tangu mapinduzi yao wenyewe.

Mohamed Bazoum - kiongozi wa kwanza kuchaguliwa nchini Niger kumrithi mwingine tangu uhuru mwaka 1960  kwa sasa anafikiriwa kuwa na afya njema, na bado anashikiliwa mateka na walinzi wake.