Alhamisi , 1st Dec , 2022

Maporomoko ya ardhi kwenye barabara ya magari kusini mwa Brazil yamesababisha vifo vya watu wasiopungua wawili na kusababisha watu kadhaa kutoweka.

Mlipuko wa tope ulianguka kwenye barabara kuu ya BR-376 katika jimbo la Paraná, na kugonga zaidi ya magari 21, mamlaka imesema.

Wafanyakazi wa uokozi katika eneo la tukio walisema hali mbaya ya hewa na eneo la mbali vinatatiza juhudi za utafutaji.

Wazima moto wanatumia kamera ya joto ili kupata manusura wanaowezekana. Takriban watu 30 wanadaiwa kutoweka.

 Picha za angani zinaonyesha lori moja likining'inia kando ya daraja. Wafanyakazi wa uokozi walipata mwili wa dereva wake, ambaye alitambuliwa kama João Pires mwenye umri wa miaka 62. 

Mashuhuda mmoja alisema alifanya kazi kama dereva wa lori kwa muda mrefu wa maisha yake na alifahamiana vyema na barabara ambako ajali hiyo ilitokea.