
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli alizipendekeza siku hizo kuwa ni kuanzia Ijumaa ya leo ya Aprili 17, 2020, hadi Jumapili ya Aprili 19.
"Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020, kumuomba Mwenyezi Mungu, aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia" alisema Rais Dkt Magufuli.