Jumanne , 21st Jul , 2020

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Seleman Jafo amesema Manispaa ya Ilala imeongoza nchi nzima  kwa ukusanyaji wa mapato Gafi kutoka bulioni 44 Hadi kufikia ziaid ya bilioni 57.

Taarifa zaidi na Donald Mtani. Mhe Jafo ametoa kauli hiyo Mara baada ya kufanya ziara katika shule za msingi Gongolamboto Jica na Mwangaza kuangalia ujenzi wa vyumba sita vya madarasa Ambapo ameridhika na ujenzi wa madarasa hayo akimpongeza mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala  na walimu kwa usimamizi Thabiti.

Mhe Jafo amesema kuwa shule hizo zilikuwa na changamoto ya vyumba wakati alipotita kukagua siku za awali huku Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala akieleza mbinu wanazotumia kukusanya mapato yanayowasaidia kutekeleza miradi kwa wakati

Wakati huo huo  Mhe Jafo ametembelea mradi wa ujenzi wa Daraja la ulongoni B ambalo lilisombwa na maji na kumtaka Mkandarasi aliyepewa Tenda ya ujenzi kulikamilisha kwa muda uliopangwa ili kuondoa adha inayowapata wananchi hasa katika kipindi Cha mvua.Daraja ambalo linatarajiwa kujengwa kwa gharama ya  shilingi Bilioni 4.5