
Kamanda Mambosasa ameyabainisha hayo leo Agosti 5 ikiwa ni kipindi cha Mkutano wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC na kwamba kuanzia kesho Agosti 6 msako mkali utaanza kufanywa na kuwakamata watakaokaidi agizo hilo na ni marufuku ya kudumu.
''Marufuku hiyo inakwenda kwa watu wote wenye magari waliyoweka alarm, isipokuwa kwa magari maalumu kama polisi na Ambulance, msako mkali unaanza kesho yeyote atakayekamatwa na hizo taa iwe urembo lakini unasababishia watu taharuki na kupaki magari na kunyimwa haki ya kutumia barabara, watakamatwa na sitowaachia mpaka watakapokuja na mafundi wao waje kuwabadilishia kituoni.'' amesema Mambosasa.
Kwa upande mwingine jeshi la polisi limepiga marufuku kwa madereva bodaboda wote, kufika mjini kwa kipindi hiki chote cha ugeni na kushauriwa waendelee kufanya biashara zao pembezoni mwa mji.