Jumatatu , 19th Oct , 2020

Wananchi wa mtaa wa Mangaya uliopo Mbagala, Jijini Dar es Salaam, wameiomba serikali kuitengeneza barabara ya Shimo la mchanga ambayo imeharibika vibaya na kushindwa kupitika kwa urahisi hali ambayo inasababisha wakati mwingine hata wajawazito kujifungulia njiani.

Sehemu ya barabara ya Mtaa wa Mangaya, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wakiongea na Kurasa leo wananchi hao wamesema kinamama wajawazito wamekuwa wakijifungulia njiani kutokana na ubovu wa barabara hiyo huku wakieleza kwamba mvua inaponyesha ndio inashindwa kupitika kabisa hali inayosababisha hata magari yanapopita kuharibika.

“Hali ya barabara hii ni mbaya sana tunapata shida sana sisi wakazi wa huku hivyo serikali ituangalie kwa jicho la huruma” amesema Zalia Habibu mkazi wa Mangaya

Amesema tayari kilio chao hicho wamekifikisha kwenye ngazi ya serikali ya mtaa na waneahidiwa kutengenezwa kwa barabara hiyo.