Jumatano , 1st Mar , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.