Jumatano , 28th Apr , 2021

Mama anayefahamika kwa jina la Noelia mkazi wa Nsemulwa shuleni, wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, amekula pesa za michango ya harusi kiasi cha shilingi 80,000 kwa kudai amejilipa mahali maana mkwe wake huyo hajawahi kumlipia mahari binti yake tangu aanze kuishi naye.

Kadi ya mchango

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya harusi hiyo wameeleza hali halisi iliyojitokeza siku ya kupanga bajeti ili wagawane majukumu ya kwenda kununua mahitaji ikiwemo vyakula na vinywaji, ndipo walipohitaji fedha hizo na hazikupatikana mpaka bwana harusi alipoingilia kati na kutoa pesa zake mfukoni.

Wakiendelea kutoa simulizi cha yaliyojiri siku hiyo ya kikao cha bajeti ,wanakamati wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na mama huyo  huku wakikiita ni mmommonyoko wa maadili ya kiafrika.

EATV ilifika nyumbani kwa wanafamilia hao kwa ajili ya  kuhojiana nao kuhusu tuhuma zinazowakabili badala yake waligoma kuzungumzia suala hilo na kuanza kurusha maneno yaliyoashiria pesa hizo zimeliwa.