Ijumaa , 4th Nov , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda amepokea jumla ya madawati 200 yenye thamani ya shilingi milioni 20 za kitanzania kutoka kwa Jumuiya ya Kislam ya Khoja Shia Ithina Asheri Jamaat ijulikanayo kama KSIJ Dar es salaam.

Madawati

Akipokea madawati hayo Mheshimiwa Makonda ameshukuru na kutoa wito kwa wanafunzi wa Jiji la Dar es salaam kusomea masomo ya Sayansi ili kwenda na kasi ya mabadiliko ya sayansi teknolojia ya ulimwengu wa leo sanjari na ari ya serikali mpya ya kujenga uchumi wa viwanda kwa kuwa taifa bado lina uhaba wa wanafunzi, walimu na wataalam waliobobea katika fani hizo.

Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya elimu ya shule ya Al Muntazir Imitiaz Lalji amebainisha kuwa siku za karibuni limetokea kundi la wazazi wachache wanaojiita ni umoja wa wazazi wenye watoto katika shule za Almuntazir na kujaribu kuchafua jina la shule kwa kuchapisha kusambaza maaandishi ya kichochezi kwa umma.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya KSIJ na Msimamizi Mkuu wa Shule za Al muntazir  Bwana Azim Dweji amemuomba Mkuu wa Mkoa kuwapa eneo lenye ukubwa wa nusu hekari kwa ajili ya ujenzi   wa shule nyingine kama hatua ya upanuzi wa utoaji huduma za elimu za shule za Almuntazir.