Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime amesema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 3 mwaka huu majira ya saa 3 usiku ambapo miongoni mwa watu waliofariki ni familia ya Mkaguzi wa polisi ambaye pia ni Msaidizi wa Inspekta Jenerali wa polisi, Gerald Ryoba iliyokuwa ikitokea Mkoani Geita kuelekea mkoani Dar es Salaam.
Kamanda Misime amesema kuwa katika ajali hiyo Ryoba alikufa yeye pamoja na mkewe aliyemtaja kwa jina la Fidea John Kiondo ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi Wilayani Temeke Mkoani Dar es Salaam, pamoja na watoto wao wawili wa kiume.
Aidha Kamanda Misime ametoa wito kwa madereva kuwa makini wanapokuwa wanaendesha magari hasa kwenye maeneo yenye maji mengi ili kuepusha maafa.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, Dk. Ibenzi Ernest amethibitisha kupokea maiti sita za watu waliokufa kwenye ajali hiyo ya maji mjini Kibaigwa.



