Jumamosi , 28th Nov , 2015

Wahudumu katika vituo vya afya mkoani Dodoma hulazimika kuchota maji nje ya vituo hivyo ili kuwahudumia wagonjwa wanaofika kupatiwa matibabu.

Foleni ya kuchoka maji ya Bomba,katika moja ya vitongoji nchini Tanzania

Wahudumu katika vituo vya afya mkoani Dodoma hulazimika kuchota maji nje ya vituo hivyo ili kuwahudumia wagonjwa wanaofika kupatiwa matibabu.

Wakiongea na East Africa Radio waganga wa wilaya za Chamwino na Mpwapwa zilizopo mkoani Dodoma kwenye kikao cha bodi ya washauri wa mradi wa Mkaji kilichokuwa na lengo la kujadili mafanikio, changamoto na jinsi ya kuzitatua mjini Dodoma.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Dk, Said Mawji amesema hali ya upatikanaji wa maji kwenye vituo vya afya wilayani humo siyo ya kuridhisha vituo vingi vya afya na zahanati vinakabiliwa na ukosefu wa maji kutokana na jiografia ya eneo vilipo kuwa na milima na hata maji yanayopatikana kuwa si safi na salama.

Naye ofisa afya wa wilaya ya Chamwino, Dk, Cathbert Kongola amesema hali ya upatikanaji wa maji katika vituo vya afya ni asilimia 50 pekee hasa upatikanaji wa maji ya uhakika kwa kuwa sehemu nyingi maji yanapatikana mbali kutokana na miundombinu ya maji kutofika kwenye vituo hali ambayo huwalazimu wananchi kubeba maji pindi wapokwenda kwenda vituo kupata huduma za matibabu.

Kwa upande wake afisa mradi wa Mkaji, Sostenes Gabriel amesema mradi huo una mpango wa kuvifikia jumla ya vituo vya afya na zahanati 100 katika wilaya zote saba za mkoa wa Dodoma ambapo katika kila wilaya watachagua baadhi ya vituo vya afya ambavyo watakarabati muindombinu ya maji na pale ambapo hakuna watajenga mipya.