Alhamisi , 9th Feb , 2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, kuchunguza ukusanyaji wa mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Waziri Mkuu akisikiliza maelezo kutoka kwa Regina Masoud kuhusu mfumo mpy wa ukusanyaji mapato, ATCL

 

Ametoa kauli hiyo leo, alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.

Waziri Mkuu amesema serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya Taifa.

Kadhalika amewataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.

Waziri Mkuu akizungumza na baadhi ya viongozi wa ATCL

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa ATCL, , Bi. Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingaria ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.