Ijumaa , 26th Dec , 2014

Kituo cha Huruma Mkoani Mara kinakabiliwa na changamoto ya kutoa malezi kwa wenye matatizo ya afya ya akili, watoto yatima na wale ambao wamekuwa wakitengwa katika familia zao, hali inayopelekea kukabiliwa na upungufu wa mahitaji muhimu

Moja ya Zawadi zilizowahi kutolewa msaada kwa vituo vya kulelea Yatima.

Kiongozi mmoja wa dini ambaye amejitolea kutoa maelezi kwa jamii hiyo Padri Godfried Biseko, akizungumza wakati wa kupokea msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na mahitaji mengine muhimu kwa jamii,

Pamoja na kushukuru kwa msaada huo, amesema tatizo la Wanawake wenye matatizo ya afya ya akili kupewa mimba na kutelekezwa kumechangia ongezeko la wahitaji katika kituo hicho.

Naye mwakilishi wa kampuni ambayo imetoa msaada huo wa vyakula na mahitaji mengine muhimu Bw. Zakayo Ngatu, amesema kampuni yake imekuwa na taratibu za kuyajali makundi yenye mahitaji ndani ya jamii kwa kutoa msaada kama huo ili kuwezesha jamii inayolelewa katika kituo hicho kusherekea siku kuu ya krismasi na mwaka mpya kama watanzania wengine.