Jumanne , 26th Jul , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge amesema hata mvumilia Mkuu wa Wilaya atakayeshindwa kuweka mikakati ya Usafi katika wilaya yake pamoja na Utunzaji wa Mazingiria.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge.

Akizugumza jana Mkoani humo mara baada ya kushiriki zoezi la Usafi ndani ya Wilaya ya songea kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Mashujaa ambapo amesema hatamvumilia mkuu wilaya hiyo endapo atashindwa kuiweka wilaya hiyo katika hali ya usafi.

Katika hatua nyingine Dkt. Mahenge amesema ukuaji wa mji unahitaji uwepo wa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo stand ya mabasi iliyobora huku akimtaka mkurugezi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea kusimamia ujenzi huo.

Wananchi walioshiriki kwa zoezi hilo wameipongeza hatua hiyo ya mkuu wa mkoa kujitokeza kufanya usafi na kutaka zoezi hilo liwe endelevu ila Manispaa hiyo iwe katika hali ya Usafi kwa muda wote na kuweza kuongoza na kipigiwa mfano nchini.