Dkt Shein ametoa kauli hiyo hapa Zanzibar wakati akihutubia katika siku ya sheria Zanzibar ambayo ilifanyika katika viwanja vya bustani ya Victoria na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria wakiwemo majaji, mahakimu, wanasheria na mawakili wakiongozwa na makamu wa pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi pamoja na Jaji mkuu wa Tanzania Omar Chande.
Dkt Shein aliwataka majaji na mahakimu kufanya kazi yao bila ya hofu na bila ya upendeleo huku akiwataka wananchi kufanya juhudi za kuzielewa na kuzifuata sheria.
Mapema katika siku hiyo ya sheria Zanzibar wakuu wa sekta hiyo muhimu za sheria walipata fursa ya kutoa salamu zao ambapo mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan alisisitiza umuhimu wa Katiba na utawala bora huku Rais wa chama cha wanasheria Zanzibar Awadh Ali Said alishauri serikali kuanzisha mfuko maalum wa utendaji wa mahakama.
Naye Jaji mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Makungu kwa upande wake amesema bado tatizo la rushwa limekuwa ni sugu ingawa mahakama imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana nayo.
Sherehe hizo za siku ya sheria Zanzibar ambazo mwaka huu kauli mbiu ni mahakama huru, msingi na utawala bora