Alhamisi , 26th Jan , 2017

Mahakama nchini Kenya imewapa madkatari na wauguzi muda wa siku tano kumaliza mgomo wao.

Madaktari nchini Kenya

 

Madaktari hao wamekuwa wakiitaka serikali iheshimu makubaliano ya mwaka 2013 ya kuwaongezea mishahara na marupurupu .

Wamekataa nyongeza ya asilimia 40 katika mishahara iliyotolewa na serikali wakidai ni ya chini kuliko ile waliyoafikiana mwaka 2013.

Takriban madaktari na wauguzi 5,000 kutoka hospitali 2000 za umma, walianza mgomo wiki ya kwanza ya mwezi Disemba ambapo wagonjwa wamekuwa wakiteseka kwa kukosa huduma za matibabu.

Jaji katika Mahakama ya ajira amesema, siku hizo tano siyo za mazungumzo bali za kumaliza mgomo.