Alhamisi , 14th Jan , 2016

Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi leo imeahairisha shauri la wakazi 681 waliojenga mabondeni wanaopinga kubomolewa nyumba zao kwanza hadi wapatiwe mahala pa kwenda.

Akizungumza mara baada ya kuhairishwa kwa shauri hilo wakili wa upande wa walalamikaji George Mwalali amesema kuwa baada ya mabishano ya kisheria kati ya mawakili wa serikali na wa walalamikaji Jaji Panterine Kente amehairisha shauri hilo mpaka tarehe 25 Januari litakaposikilizwa tena.

Kwa upande wake mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia amewataka wakazi hao wa mabondeni ambao wanapinga kubomolewa nyumbani zao kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo wawakili wanaowatetea wanafanya kazi ya kuhakikisha shauri lao hilo linakwisha kwa wao kupata ushindi.

Wakazi 681 wa mabondeni wanapinga nyumba zao kubomolewa huku wakiitaka serikali kuwapa makazi mbadala kabla ya kuwavunjia kwa nyumba zao huku baadhi wakiwa na hati na leseni za makazi.