Maonesho hayo ya biashara yajulikanayo kama maonesho ya sabasaba yanayofanyika kitaifa Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Akizungumza na Waaandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mheshimiwa Charles Mwijage amesema kuwa Rais huyo wa Rwanda ndiye atakuwa mgeni rasmi na mfunguzi mkuu wa maonesho hayo ambayo yamezikutanisha nchi 30 kutoka mataifa mbalimbali duniani zilizokuja kuonesha bidhaa na teknolojia zao.
Mheshimiwa Mwijage amesema kuwa maonesho ya mwaka huu ni ya kipekee ukilinganisha na yale ya miaka ya nyuma kwani ndiyo maonesho ya kwanza ambayo yanafanyika wakati serikali inapoanza mpango wa pili wa maendeleo ya miaka mitano wenye dhima ya ujenzi wa uchumi wa viwanda unaolenga kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.
Aidha Mwijage ametoa wito kwa watanzania wenye ndoto ya kuwa na viwanda kutembelea maonesho ya sabasaba ili wajifunze kutoka kwa wataalam wa ujenzi wa uchumi wa viwanda namna wanavyoweza kuanzisha viwanda na kuwekeza katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa.




