
Kushoto ni Dkt. Bashiru Ally katibu mkuu CCM na na Rais Magufuli.
Mwenyekiti huyo wa CCM ameeleza hilo leo kwenye hotuba yake wakati wa mapokezi ya ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyowasili nchini mchana wa leo Januari 11, 2019 kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
''Dkt. Bashiru amekuwa muwazi, huwa namuangalia kwenye hotuba zake saa nyingine nasema kumbe mimi nafuu bwana kuliko huyu jamaa'', amesema.
Rais ameeleza kuwa Katibu wake huyo amekuwa akikemea ufisadi ambao ulikuwa ukishamili siku hadi siku lakini sasa yeye anapingana nao hadharani bila kujali.
Magufuli amewataka viongozi wote wa chama na Serikali kuendelea kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja ili kusaidia maendeleo na siku moja Tanzania itakuwa kama Ulaya.