Jumanne , 9th Jun , 2015

Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuri ambaye pia ni miongoni mwa wagombea waliochukua formu za kuwania mbio za uraisi wa awamu ya tano amesema hawezi kuthubutu kuzungumza chochote mbele ya hadhara ya wananchi.

Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuri ambaye pia ni miongoni mwa wagombea waliochukua formu za kuwania mbio za uraisi wa awamu ya tano amesema hawezi kuthubutu kuzungumza chochote mbele ya hadhara ya wananchi katika kipindi hiki kigumu cha kutafuta wadhamini na kwamba kufanya hivyo nikukiuka maadili ya chama chake.

Akizungumza mjini Bukoba wakati wa akitoa shukrani zake kwa waliojitokeza kumdhamini, waziri Magifuli amewaambia wadhamini wake mkoani Kagera kwamba hawezi kuongea kitu chochote juu ya nini atawafanyia wananchi endapo atachaguliwa kushika nafasi ya urais wa awamu ya tano na kuongeza kuwa muda wa kufanya hivyo bado haujafika kwa kuwa kampeni hazijaanza, hivyo wanaotoa ahadi wanakiuka kanuni za chama.

Naye, Profesa Mark Mwandosya ameonesha kutoridhishwa na baadhi ya taratibu zilizowekwa na chama hicho zinazowazuia wagombea wa nafasi ya urais kuomba kura kwa wajumbe wakati huu wanapoendelea na mchakato wa kutafuta wadhamini.