Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Salum Hapi
Akizungumza leo kwenye Hafla ya kuapishwa kwa wakuu wa Wilaya za Dar es Salaam, Mkuu huyo wa Wilaya Bw. Ali Salum Hapi amesema kuwa suala hilo licha ya kutaka msaada kutoka serikalini lakini na wadau washiriki ili kuweka mazingiria mazuri kwa wanafunzi wa wilaya kupata elimu bora.
Bw. Hapi amesema wameamua kwenda mbali zaidi katika kuweka mazingira safi ya Elimu katika wilaya hiyo ili iwe ya kupigiwa mfano kwa wilaya zote ambayo itakua na mazingira mazuri ya katika utoaji elimu kupitia sera ya Elimu bure.
Katika hatua nyingine amezungumzia mikakati ya utunzaji wa mazingira katika wilaya yake ambapo amesema kila mfanyabishara katika wilaya hiyo aweke na kifaa cha kutunzia uchafu katika maeneo yake ya biashara ili kupunguza tatizo la kuzagaa kwa taka.








