Mabasi yaliyofutiwa kuanza safari saa 9 usiku
katika vituo vya mabasi na kwamba basi lililoshinda lilimwagiwa maji na kushangiliwa
Mabasi hayo ni sita (6) ya Ally's Star (T946 EBF, T947 EBF, T948 EBF, T354 DXS, T357 DXS na T360 DXS) na matatu (3) na Katarama Express (T835 EBR, T836 EBR, T212 ECR) na endapo wataendelea kukiuka maelekezo leseni zao zitafutwa.
Aidha kampuni ya Isamilo, kwa kuwa matukio yake hayajakithiri, pamoja na watoa huduma wengine wanaofanya mchezo huu, wamepewa onyo kali na la mwisho kabla hawajachukuliwa hatua stahiki.
Mbali na hayo madereva na wamiliki wa magari wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utoaji huduma za usafiri wa umma.