Jumatano , 21st Sep , 2022

Mabaki ya mwili wa mwanafunzi, Levis Mwailemale (16) wa kidato cha nne katika  shule ya sekondari Ikuti iliyoko wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, aliyepotea zaidi ya miezi nane iliyopita yamekutwa porini pamoja na nguo alizokuwa amevaa wakati anapotea.

Levis Mwailemale, enzi za uhai wake

Familia imeeleza kuwa kijana Levis Mwailemale alipotea katika mazingira ya kutatanisha Januari 9 mwaka huu, ambapo walianza jitihada za kumtafuta bila mafanikio  hadi Septemba 18 walipokuta mabaki ya mwili wake.

Hata hivyo  maziko ya mwili wa kijana huyo  yalifanyika baada ya Jeshi la Polisi kukamilisha uchunguzi wake na kutoa kibali.