Maandamano hayo yameitishwa ya chama cha wafanyabiashara na vyama vingine kufuatia kile kilichoelezwa kukiukwa kwa haki na uhuru kulikoonekana dhahiri katika upigaji wa kura hiyo ya maoni iliyopigwa jumapili.
Mamlaka nchini humo ilisema kwamba kura hiyo haikuwa halali hata hivyo zaidi ya watu milioni 2.2 walipiga kura katika zoezi hilo lililofanyika jumapili pamoja nakukabiliwa na vyombo vya usalama vilivyotaka kusimamisha zoezi hilo na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa.
Inasemekana baadhi ya maafisa wa polisi walitoa amri ya kuzuia watu wasipige kura na walionekana wakipiga risasi za mpira na kuvamia vituo vya kupigia kura ikiwa ni pamoja na kuwavuta wanawake nywele zao.