
Mshauri wao Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital leo Agosti 24, Katibu Msaidizi wa kamati ya itikadi, uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ATC Seif Suleimani, amesema Jeshi la polisi lilifika na kumzuia Mshauri Mkuu kufanya uzinduzi.
''Jeshi la polisi kutuzuia kufanya shughuli zetu kuu za msingi za kisiasa ni kutuingilia NA kuingilia uhuru wetu wa chama cha siasa, na tunalitaka jeshi la polisi mara moja liache kutuingilia katika kufanya shughuli zetu za kisiasa'' amesema Seif.
Aidha kiongozi huyo amesema chama hicho kinafanya shughuli ya uzinduzi wa matawi mapya ikiwa ni hatua ya kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa kama vyama vingine vya siasa vinavyofanya.
#HABARI @ACTwazalendo
kimeeleza kuwa Polisi Temeke wamezuia kikao kilichokuwa kihutubiwe na Mshauri wao Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad katika ofisi ya ACT kata ya Azimio. Wanachama wameamriwa kutawanyika huku Katibu wa kamati ya uadilifu ya chama Maharagande Mbarala akikamatwa. pic.twitter.com/ndGZb3buTe— East Africa TV (@eastafricatv) August 24, 2019