Mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad.
Seif ameyasema hayo leo Oktoba mosi, wakati akifanya kampeni zake Pemba ambapo amesema kuwa Zanzibar imebarikiwa mafuta na gesi asilia na kuahidi kuwa atahakikisha anaweka sera nzuri ili kusaidia kukuza uchumi.
''Zanzibar tuna mafuta na gesi asilia,tuna sera ya mafuta na gesi na wale wote ambao ardhi zao zimechukuliwa au kuathiriwa na gesi lazima walipwe fidia ambayo inatosha kabisa"amesema Maalim Seif.
Mgombea huyo ameongeza kuwa atahakikisha anawatengenezea wazanzibar mamlaka kamili ya nchi yao na pia kujenga uchumi ambao utaleta huduma nzuri za kijamii.
"Ahadi ya kwanza ni kuwatengenezea wazanzibar mamlaka kamili ya nchi yao,Tutajenga uchumi maisha ya raha na furaha,huduma nzuri za kijamii ikiwemo afya,elimu,usafiri na usafirishaji"amesema Maalim Seif
Aidha amesema kuwa atahakikisha haki moja kubwa anaitimiza ambayo ipo katika katiba ya kila mtu kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa.