Viongozi wa CHADEMA walioakamatwa
Lissu, Mnyika na Sugu wamewasili Mbeya hii leo Agosti 11, 2024, kwa ajili ya kuungana na vijana wa BAVICHA kushiriki kongamano la maadhimisho ya vijana duniani lililokuwa limeandaliwa na vijana ndani ya chama hicho.
Mapema leo Jeshi la polisi nchini limepiga marufuku maandamano au mikusanyiko ya aina yoyote ile inayotaka kufanyika kwa mwamvuli wa kuadhimisha siku ya vijana duniani kwa mkoa wa Mbeya kwa sababu yamelenga kuvunja amani na utulivu wa Taifa.