
Wagombea wa nafasi ya Urais na Makamu wa Rais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu.
Hayo yamejiri hii leo Agosti 25, 2020, wakati wa kuhitimishwa kwa zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za uteuzi kwa nafasi za Ubunge, Udiwani na Urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), lililoanza Agosti 5, 2020, ambapo takribani vyama 17 vyenye usajili wa kudumu na vyenye sifa vilisimamisha wagombea wa Kiti cha Urais.
Wagombea wengine waliopitishwa na NEC hii leo, ni pamoja na John Mgufuli kupitia CCM, Hashim Rungwe kupitia CHAUMMA, Bernard Mende kupitia ACT Wazalendo, John Shibuda kupitia chama cha ADA-TADEA, Khalfan Mohamed Mazurui kupitia chama cha UMD, Leopold Mahona kupitia chama cha NRA.
Wengine ni Seif Maalim Seif wa chama cha AAFP, Queen Cuthberta Sendiga kupitia chama cha ADC, Philipo John Fumbo wa chama cha DP, Profesa Ibrahim Lipumba kupitia CUF, huku mgombea wa chama cha CCK na chama cha NLD wakikatwa kwa kushindwa kutimiza vigezo vya NEC.
Mara baada ya zoezi hili kukamilika, wagombea wote ambao wameteuliwa wataanza kufanya kampeni rasmi kuanzia kesho Agosti 26, 2020.