
Haji Juma a.k.a Prince Haji
Prince ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani katika jimbo la Manchester new Hampshire akifanya vizuri na kundi la Afro Band amesema yupo Marekani kimuziki lakini amesema mambo yakienda vizuri amepanga kuanzisha bendi mwezi wa sita mkoani Kigoma ikiwa ni pamoja na kusaidia watoto yatima.
''Nimeanza muziki miaka miwili iliyopita na nia na madhumuni yangu mimi kufanya muziki nikiwa na lengo kubwa la kusaidia watoto yatima ''Amebainisha Prince Haji.
Kwa sasa Mwanamuziki huyo ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ''kupenda'' wimbo ambao amesema unahusu mapenzi anamuelezea mpenzi wake juu ya mapenzi aliyonayo kwake.
Sikiliza hapa

