Jumatano , 12th Jan , 2022

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, amesema atahakikisha anafuatilia ripoti kutoka jeshi la polisi, itakayotoa taarifa za ukweli ili kujua ni nini kinachopelekea wanahabari kuguswa zaidi pindi ajali za magari ya misafara ya viongozi zinapotokea.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye,

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 12, 2022, jijini Mwanza, alipohudhuria zoezi la kuagwa kwa miili ya wanahabari, waliopoteza maisha hapo jana mkoani Simiyu, katika ajali ya gari lililokuwa katika msafara wa viongozi wa mkoa wa Mwanza waliokuwa wakielekea Ukerewe kwenye ukaguzi wa miradi.

"Tupitie ajali zote zilizohusisha wanahabari kwenye misafara, viongozi wangu wameniagiza tuwaombe wenzetu wa jeshi la polisi watuletee ripoti za ajali hizi, tuzipitie tuone kwanini zinagusa wanahabari na tuchukue hatua ya kuwalinda wanapotimiza wajibu wao kwenye misafara ya viongozi wetu," amesema Waziri Nape