
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Yamungu Kayandabila wakati akiongea na East Africa Radio nakusema kuwa idadi hiyo inaonyesha ukubwa watatizo la migogoro ya ardhi nchini ambapo wizara yake imejipanga kuanzisha mfumo mpya wa utendaji kazi kwa kuunga mfumo wa taarifa zake kwa nchi nzima kwa lengo la kuondoa migogoro hiyo.
Dk. Kayandabila amesema mfumo huo utatoa suluhu ya kuwepo kwa umiliki wa watu wawili na zaidi katika kiwanja kimoja, malipo ya hati ya ardhi na malipo ya kodi ya ardhi na kuwezesha kila mwananchi kupata taarifa zote muhimu za wizara hiyo katika maeneo yao.
Dk. Kayandabila ameongeza kuwa kwa mkoa wa Dar es Salaam Wilaya ya Kinondoni inaongoza kwa kuwa na migogoro mingi ya ardhi ya makazi na umiliki wa kiwanja kimoja kumilikiwa na watu zaidi ya 3 na kuahidi kutatua migogoro hiyo ndani ya miaka 5.