Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kufikia Machi 30 kipindupindu kiwe historia-Ummy

Jumatano , 3rd Feb , 2016

Viongozi wote kuanzia ngazi ya vijiji wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu hadi kufikia tarehe 30 Machi mwaka huu

Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu

Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipokutana na kikosi kazi cha cha udhibiti wa kipindupindu mkoa wa Dodoma

"Kipindupindu siyo suala ya afya peke yake, bali ni suala mtambuka hivyo sekta zote zinapaswa kujumuika katika kupambana na kutokomezwa ugonjwa huu"

Ummy amesema kipindupindu bado ni changamoto na ni janga hivyo kila mkoa unatakiwa kuliwekea kipaumbele kwakuwa ugonjwa huo unaua kwa haraka hivyo viongozi wote washiriki kikamilifu na si kuwaachia waganga.wakuu wa mikoa au wilaya

Aidha amesema licha ya kuwa na sheria ndogo Za kila halmashauri za kusimamia usafi na mazingira lakini katika kudhibiti kuenea kwa kipindupindu lazima litakuja suala la kufungia biashara hususan za mbogamboga, matunda pamoja na chakula

"Suala la kukusanya mapato lipo na litaendelea kuwepo lakini suala la kipindupindu linapoteza maisha, maisha hayatafutwi lakini pesa zinatafutwa lakini ukikosea utapoteza maisha ya watu wengi"

Ummy amesema tangu kipindupindu kiingie nchini Agosti mwaka jana, halmashauri zimetumia pesa nyingi katika kutokomeza ugonjwa huo, lakini wangeweza kuzuia mapema, pesa hizo zingeenda kutatua tatizo la madawati katika shule za msingi nchini.

"Mnapoona hamjaridhika na uendeshaji wa migahawa,msisite kuzifungia mara moja, mapato mtakusanya haraka kwa kuwa na nguvu za pamoja baada ya kutokomeza ugonjwa na kuweza kuingiza mapato mengi na kwa haraka tofauti na kuwa na hilo tatizo.

Hatahivyo amevizitaka vikosi vyote vya mikoa nchi, kuwashirikisha wadau wote wakiwemo viongozi wa dini zote kuweza kuelimisha kutoa elimu ya jinsi gani ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa waumini wao.

Mkoa wa Dodoma umetumia takribani shilingi milioni 124 za kitanzania toka kipindupindu kiingie na hadi leo kuna wagonjwa wanne katika kambi ya kipindupindu wilaya ya Bahi.

Jumla ya wagonjwa 450 waliugua na vifo12, wilaya zilizoathirika ni Bahi, Dodoma mjini na Chamwino

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea