Jumatano , 18th Feb , 2015

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wanaojihusisha na ulinzi wa watoto leo watazindua rasmi kongamano la kitaifa la siku tatu ili waweze kutafakari utekelezaji wa mpango kazi wa huduma kwa watoto walio katika mazingira magumu.

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya Dkt, Donan Mbando.

Taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu wa Wizara ya Afya Dkt, Donan Mbando amesema kongamano hilo linafanyika hapa nchini Tanzania kwa kuzingatia hali halisi ya watoto hao kama tafiti mbalimbali zinavyoonesha hapa nchini.

Kwa mujibu wa utafiti wa hali ya Afya na watu Tanzania uliofanyika mwaka 2010 umebaini kuwa Tanzania ina watoto Milioni 2.5 yatima na wengine walioko katika mazingira hatarishi wanatokana na Ukimwi na VVU.

Aidha utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2011 Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 75 ya watoto wote Tanzania ni wahanga wa vitendo vya ukatili huku kati yao asilimia 30 ya wasichana na asilimia 13 ya wavulana wameshafanyia ukatili kingono katika utoto.

Aidha utafiti mwingine ulifanywa na umoja wa Mataifa mwaka 2013 unayonyesha kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi zenye idadi kubwa ya mimba za utotoni ambazo husababusha wasichana kukatisha masomo yao.