Alhamisi , 11th Feb , 2016

Kivuko cha Mv Kigamboni jijini Dar es salaam asubuhi ya leo kimepata hitilafu na kuzua taharuki kwa abiria waliokuwamo

Wakazi wa Kigamboni jijini Dar es salaam wameitaka serikali kuboresha huduma za kivuko kinachosafirisha abiria kutoka Kigamboni kuelekea Feri katika ufukwe wa bahari ya Hindi kutokana na kivuko hicho kukwama mara kwa mara na kuleta adha kwa wakazi wa eneo hilo.

Wakazi wa eneo hilo wamelalamikia kivuko hicho kukwama na kupelekea kuhofia usalama wao baada ya kushindwa kufika ufukweni na kuwalazimu kushuka ndani ya maji.

Baadhi yao wamesema kinachofanyika ni hujuma kwa watendaji wa kivuko hicho kwa kuiba mafuta licha ya kushindwa kufanya ukarabati wa kivuko hicho.

Wanafunzi wanaosoma shule zilizopo Kigamboni wanasema hali hiyo imewaathiri kwa kiasi kikubwa hali inayopelekea kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.