Jumatatu , 6th Jun , 2022

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesema kwamba hali ya kipupwe haitawaacha nyuma wakazi wa Dar es Salaam ambapo hali hiyo inatarajiwa kufikia 19°C, mkoa wa Njombe ni 06°C na Rukwa 09°C.

Mkurugenzi mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi

Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo umetolewa hii leo Juni 6, 2022, na kueleza kuwa vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga, visiwa Mafia, Dar es Salaam na visiwa vya Unguja na Pemba.