Alhamisi , 17th Oct , 2024

Mkazi mmoja mkoani Lindi amefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu huku wengine 24 wakiendelea kupatiwa matibabu mara baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo.

Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa mkoa wa Lindi Heri Kagya, wakati akizungumza na wanahabari juu ya mwenendo wa ugonjwa huo ambapo ameeleza wagonjwa hao wamebainika katika kijiji cha Zinga Kibaoni kilichopo Kata ya Miguruwe wilayani Kilwa huku sababu zinazopelekea kuenea kwa ugonjwa huo ni uchafuzi wa mazingira na changamoto ya majisafi na salama.

Hii inakuwa ni mara ya pili kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu mkoani Lindi, ambapo kwa mara ya kwanza uligunduliwa mwezi Juni na takribani wakazi 163 waligunduliwa kuuugua.