Jumatano , 17th Jul , 2024

Kiongozi wa mbio za Mwenge nchini, Godfrey Eliakimu Mzava, ameteketeza dawa za kulevya aina ya mirungi kg 50 na bangi zilizokamatwa wilayani Kiteto kwa matukio tofauti yakiwemo usafirishaji na hata kulimwa.

Bangi zikiteketezwa

Kaimu OCCID Kiteto Evarist Tarimo akitoa taarifa za dawa hizo amesema kiasi hicho ni sehemu tu ya dawa hizo za kulevya kwani zimekuwa zikilimwa kwa kificho na baadhi ya watu wasio waadilifu

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Njoro wakati wa uteketezaji, kiongozi huyo wa mbio za Mwenge amesema kitendo hicho hakikubaliki na kinahitajiwa kukemewa.