Jumamosi , 20th Jun , 2015

Serikali imetakiwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima zikiwemo sherere mbalimbali, ili kubana fedha kidogo zilizopo zielekezwe kwenye kukamilisha na kuibua miradi ya maendeleo ya wananchi.

Serikali imetakiwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima zikiwemo sherere mbalimbali, ili kubana fedha kidogo zilizopo zielekezwe kwenye kukamilisha na kuibua miradi ya maendeleo ya wananchi, kwani asilimia kubwa ya fedha zinazotengwa kwenye makadirio ya bajeti ya serikali kushindwa kuzifikia halmashauri nchini.

Akihutubia mamia ya wakazi wa Karumuhwa Nyang'hwale mkoani Geita kwenye mkutano wa hadhara, katibu mkuu wa CCM taifa Abdulrahman Kinana,amesema katika maeneo mengi aliyofanya ziara nchini,kilio kikuu kimekuwa ni fedha zinazotengwa kwenye bajeti,kutokufika kikamilifu kwenye halmashauri,hatua inayopelekea miradi mingi ya maendeleo wananchi kutokukamilika kwa wakati.

Katibu wa NEC itikakadi na uenezi amewataka wananchi wa wilaya hiyo,kujiepusha na vishawishi vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na baadhi ya vyama vya siasa, huku akimtaka mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo kuachia ngazi kwa kushindwa kuonyesha njia kama kiongozi mkuu wa chama cha siasa.

Amesema "Mbowe anapaswa kujiuzulu uenyekiti wa chama kwa heshima ya chama chake, amehukumiwa kwenda jela, mahakama imemuhukumu na imethibitika kuwa alikosea, hana sifa tena za kuendelea kuwa mwenyekiti, ni vema awaachie wengine"

Katibu mkuu huyo wa CCM akiwa katika wilaya mpya ya Nyang'hwale mkoani Geita, amewahakikishia wananchi,kupata mawasiliano ya simu za mkononi kwa kata nane za wilaya hiyo, katika mwaka wa fedha 2015 2016,huku kata zingine zikipangiwa kupata huduma hiyo katika mwaka wa fedha 2016/2017 na kuwashauri watendaji na viongozi wakuu wa wilaya hiyo kupima maeneo ya wilaya hiyo ili kuepuka ujenzi holela wa makazi ya wananchi.