Jumanne , 4th Jan , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba mara baada ya kuapishwa kuna mtu alimfuata kumpa hongera na mpole huku akimsisitiza kwamba mtu wa kwanza kumpinga atatoka ndani ya chama chake na sio mpinzani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 4, 2022, Ikulu ya Dar es Salaam, wakati akipokea taarifa ya utekezaji wa matumizi ya fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko- 19 Ikulu Dar es Salaam.

"Mtu mmoja aliniambia, atakayekusumbua kwenye kazi yako na uongozi wako, ni shati ya kijani mwenzio na sio mpinzani, mpinzani atakutazama unafanya nini, ukimaliza hoja zao hawana maneno, anayetazama mbele 2025 na 2030 huyu ndiyo atakayekusumbua na ndicho kinachotokea, " amesema Rais Samia.

Tazama video hapa chini