Alhamisi , 23rd Mar , 2023

Kijana mmoja aliyefahamika kwa majina ya Eliya Zabroni Shilinde mkazi wa Gongolamboto amejitokeza kuwaomba wadau,wafadhili msaada kutokana na changamoto ya kiafya aliyonayo kwenye mwili wake kwa takribani miaka sita kutokana na kupata aleji ya dawa alizomeza kutokana na maumivu ya kichwa

Eliya Shilinde ajitokeza kuomba msaada wa matibabu.

Akizungumza kwa tabu kijana huyo akikatisha maongezi kutokana na miwasho mikali mwilini mwake akibainisha kuwa anapata tabu ya kutokana na miwasho kuacha mabaka na ngozi kubanduka.

Kijana huyo amesema kutokana na uduni wa familia yake yuko na mama yake mzazi asiye na uwezo n kwamba anatamani kupata msaada kutoka kwa watanzania watakaoguswa na madhira anayopitia.

Mama mzazi anasema Eliya ni mtoto wa tatu kwenye familia yake baada ya mumewe kufariki Eliya akiwa na matatizo hayo mwaka wa tatu ameeleza kuwa imemlazimu kuacha kazi ili kumsaidia kijana wake akimwogesha na kumpa huduma zote licha ya kuwa na jinsia tofauti na yeye.

Waswahili wanasema hujafa hujaumbika eliya alikuwa mzima na sasa anapitia madhira magumu huku hali ya maisha ikiwa tete kijana wa kiume akifanyiwa huduma zote za kiafya na mama yake mzazi nani kama mama.